YANGA YASHINDA GOLI 4 HUKU CHIRWA AKIPIGA HAT trick DHIDI YA NJOMBE MJI.

HABARI ZA MICHEZO

Klabu ya yanga leo imeibuka na ushindi wa goli 4-0 ya Njombe Mji. Ushindi huo umeifanya klabu ya Yanga kuwa na point 34. Magoli yote katika mchezo huo yamepatikana katika kipindi cha pili na wafungaji wakiwa ni Obrey Chirwa goli tatu (Hat trick na Emanuel Martine .

  Wakati Obrey Chirwa akiipatia klabu yake ushindi huo yeye pia ameiga hat trick yake ya pili katika msimu huu na kuifanya ligi kuu kuwa na hat trick 2 tu tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi ambapo Chirwa kafikisha Hat Trick mbili (2) na moja ikifungwa na Emanuel Okwi.

  Chirwa kwa sasa amefikisha magoli 10 nyuma ya kinara wa magoli Emanuel Okwi ambaye mpaka sasa amecheka na nyavu mara 12 huku nyuma ya Chirwa kukifatiwa na nnahodha wa Simba John Bocco mwenye magoli 9. Swali la kujiuliza ni kuwa   je,  nani kuibuka kinara wa ufungaji msimu huu ?

   Imeandaliwa: Misangle Samweli
                              0659116814/0625954293


Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NA MCHE YANARNDELEA .

BEBI MADAHA NA ISABELA WAHUSISHWA NA KUSAGANA

YANGA KUJA NA JEZI HIZI MSIMU 2017/2018.