Posts

SIMBA SC HAPA NDIPO KAMBI YA PRE SEASON ITAPOKUWA .

Image
HABARI ZA MICHEZO ... ๐Ÿšจ || RASMI, IMETHIBITISHWA: ☑️ Simba SC๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ kuweka kambi ya Pre-season nchini Uturuki ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ท Klabu ya Simba SC imetangaza kuwa itaweka kambi ya Wiki tatu Nchini Uturuki ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ท kwaajili ya kujiandaa na Msimu Mpya wa Mashindano wa 2023/24. Wachezaji wote waliosajiliwa na Simba na wale wa zamani watakuwa sehemu ya Kambi hiyo huku wakitarajia kucheza Michezo mitatu dhidi ya timu za Uturuki ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ท kabla ya kurejea Nchini Mwishoni mwa mwezi huu. #sam_misangletz  Whatsap  : +255629552663 

MSHAHARA WA MESSI INTER MIAMI HUU HAPA SASA .

Image
HABARI ZA MICHEZO. Mmiliki mwenza wa klabu ya Inter Miami, Jorge Mas amethibitisha kuwa mshambuliaji mpya klabuni hapo Lionel Messi atapokea mshahara kati ya euro milioni 45-55 kila mwaka . "Mazungumzo yalidumu kwa miaka mitatu, ikijumuisha mwaka mmoja na nusu wa mazungumzo makali sana" MESSI PIA ATAPOKEA:  ▪️Asilimia kadhaa ya mauzo ya jezi za klabu hiyo.  ▪️Sehemu kwenye usajili wa Apple TV ya MLS ▪️Hisa za Franchise baada ya kustaafu. NB: Mshahara huo wa Messi kwa mwaka ni kati ya Tsh bilioni 119 mpaka Tsh bilioni 145 kwa mwaka. ✍️ Hata hivyo mshahara huo wa Messi ni kiduchu sana ukilinganishwa na mshahara wa hasimu wake wa muda mrefu, Cristiano Ronaldo anayelipwa Tsh bilioni 530 kwa mwaka huko Al Nassr FC ya Saudi Arabia. Via #kitengeMaulid #sam_misangletz 

NEWCASTLE UNITED WAMWAGA PESA KUFURU BIL. 183

Image
HABARI ZA MICHEZO #MICHEZO Klabu ya Newcastle United ya Ligi Kuu England EPL imekamalisha usajili wa kiungo Sandro Tonali kutoka AC Milan ya Italia kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 60 zaidi ya Bilioni 183 na milioni 999 kwa pesa ya Tanzania. Tonali raia wa Italia ana umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka 5 kujiunga na Newcastle United. Tonali ameweka rekodi kuwa mchezaji ghali zaidi aliyenujuliwa na Newcastle akivunja rekodi ya Alexander Isak ambaye alijiunga na Newcastle kwa dau la Pauni milioni 55 akitokea Real Sociedad.  Huu ni usajili wa kwanza kwa Newcastle United kwenye dirisha hili kubwa la usajili kuelekea msimu ujao wa 2023-24. #NewcastleUnited #SandroTonali

SIMBA SC WAACHANA NA JONAS MKUDE

Image
HABARI ZA MICHEZO : THANK YOU IMEENDA KWA JONAS MKUDE . KUPITIA KURASA ZAO SIMBA SC WAMEANDIKA KUWA  : Uongozi wa klabu unatoa shukrani za dhati kwa mchango mkubwa aliotoa kwenye timu yetu kiungo mkabaji, Jonas Mkude katika muda wote wa miaka 13 aliyodumu nasi. Tunamtakia kila la kheri kwenye changamoto mpya ya maisha ya soka nje ya Simba. Taarifa zaidi Simba App #WenyeNchi #NguvuMoja By : Sam_Misangle Whatsap  : +255629552663

MAYELE NA YANGA MAMBO SAFI KABISA

Image
HABARI ZA MICHEZO : TETESI ZA SOKA MITAA YA JANGWANI . Za chini ya Kapeti jioni ya leo kutoka kwenye kikao ni kuwa Mayele ataendelea kutetema ndani ya #nbcpremierleague  baada ya kukubaliana  kuongeza tena Miaka Miwili na sasa atalipwa milioni 28 kwa mwezi na kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika Ligi kuu Tanzania. Mayele amemzidi Azizi Ki anayelipwa milioni 24 kwa mwezi. Msiyempenda bado yupo.

MAN CITY NA B'MUNICH VITA KALI JUU YA WALKER .

Image
HABARI ZA MICHEZO : NANI KUMSAJILI WALKER KATI YA MAN CITY KUMBAKIZA AU BAYERN MUNICH . Beki wa Manchester City, Kyle Walker yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa EPL, FA na Klabu Bingwa Ulaya licha ya kutakiwa na Bayern. Bayern wanamuhitaji sana Walker lakini Man City wanamuhitaji zaidi beki huyo wa Uingereza. #WasafiSports By: Sam_Misangle Whatsap  : +255629552663 

YANGA NA MORISONI WAMALIZANA USIKU HUU.

Image
HABARI ZA MICHEZO : YANGA WAACHANA RASMI NA WINGA BENARD MORISON . KUPITIA UKURASA WAO WA INSTAGRAM YANGA WAMEANDIKA KUWA : ๐—ง๐—›๐—”๐—ก๐—ž ๐—ฌ๐—ข๐—จ Bernard Morrison  "Tunamshukuru Morrison kwa mchango wake katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya Young Africans SC. " #TimuYaWananchi  #DaimaMbeleNyumaMwiko

HERSI: YANGA SC IPO IMARA .

Image
HABARI ZA MICHEZO :  HERSI: YANGA SC IPO IMARA  Tunajua nini tunafanya sisi Kama Viongozi licha ya maneno yote haya ambayo mnayaona kwenye mitandao,,magazeti kuhusu sisi Viongozi na kushambuliwa kwa timu yetu Yanga.Tunajua ni kwasababu tu ya watu fulani ambao hawapendi kuona Yanga tulipo kwa sasa. Niwaombe tu kitu kimoja Kutoka kwa wanachama wetu na mashabiki wote wa Yanga,Tuendele kuwa watulivu sisi Viongozi wao tunajua nini tunafanya,Wanachama ambao watakaopata nafasi ya kuja kwenye mkutano jumamosi hii tunawaomba sana waje tuendelee kushirikiana kwa pamoja kuijenge timu hii na kufanya mkutano huu Kama katiba yetu ya Yanga inavyotaka tufanye. Bado tupo Kwenye mabadiliko na haitoshi bado tunaendelea kuijenga timu kwa gharama yoyote ile ili Yanga iwe imara leo na kesho,Ndugu zangu wanayanga wote nawaomba muwe watulivu muda wetu utapofika kila mtu atafurahi tumejipanga vyema sana. By: Misangletz. Whatsap  : +255629552663 

YANGA NA KAZE MAMBO MAGUMU

Image
HABARI ZA MICHEZO :  KOCHA Msaidizi wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze amekataa kusaini mkataba mpya wa timu hiyo, akitoa masharti magumu kwa uongozi ulioanza mazungumzo ambao ulitarajiwa kukutana jana usiku kuacha mchakato wa kumpata kocha mkuu mpya. Mkataba wa Nabi na Kaze ulimalizika Jumatatu hii mara baada ya mchezo wa Fainali ya Kombe la FA kumalizika kwa Yanga kutwaa taji hilo kwa kuwafunga Azam FC bao 1-0 lililofungwa na Kennedy Musonda uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mmoja wa Mabosi wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ameliambia Championi Ijumaa kuwa, jana mazungumzo yalishindwa kufikia muafaka mzuri kati ya uongozi na Kaze ambaye ameomba afanyiwe maboresho katika mkataba wake mpya. Bosi huyo alisema kuwa kikubwa ameutaka uongozi wa timu hiyo, kuongeza ofa ya kuongeza mkataba na mshahara ambayo ni siri aendelee kubakia hapo Jangwani. Aliongeza kwa kutoa sharti la kuchukua dau hilo la kumbakisha na mshahara huo, lakini awe kocha mkuu na sio msaidizi kama ilivyokuwa awali. “Mar

TETESI : KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA

Image
HABARI ZA MICHEZO :  TETESI: KOCHA MPYA YANGA SC Baada ya kuondoka kocha Nabi, klabu ya Yanga imeanza mazungumzo ya mkataba na Miguel รngel Gamondi. Miguel ni  kocha kutoka Argentina anayekinoa kikosi cha Ittihad Tanger (Morocco).  Kocha huyo ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika kwani kashawahi kuwa kocha mkuu katika klabu za Mamelodi Sundowns, USM Alger, Wydad Casablanca, Platinum Stars na CR Belouzidad. Gamondi pia kashawahi kuwa kocha msaidizi timu ya taifa ya Burkina Faso na Esperance Sportive de Tunis.